// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SERENGETI GIRLS YATOLEWA KUFUZU KOMBE LA DUNIA KWA VIPIGO ‘DABO’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SERENGETI GIRLS YATOLEWA KUFUZU KOMBE LA DUNIA KWA VIPIGO ‘DABO’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
    Saturday, March 15, 2025

    SERENGETI GIRLS YATOLEWA KUFUZU KOMBE LA DUNIA KWA VIPIGO ‘DABO’


    TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Girls imetupwa nje ya mbio za kuwania tiketi ya Kombe la Dunia 2025 baada ya kufungwa 1-0 na wenyeji, Zambia ‘Copper Princesses jioni ya leo Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola.
    Bao la Copper Princesses leo limefungwa na Natasha Nkaka dakika ya 53, hivyo wanasonga mbele Raundi ya Tatu na ya mwisho ya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Morocco kuanzia Oktoba 17 hadi Novemba 8, mwaka huu kwa ushindi wa jumla 4-0 na watakutana na mshindi wa jumla kati ya Benin na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
    Ikumbukwe mechi ya kwanza Serengeti Girls ilifungwa 3-0 na Zambia Jumapili iliyopita Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam — mabao ya Copper Princesses yakifungwa na Grace Phiri dakika ya 64 na Mercy Chipasula mawili, dakika ya 80 na 89  kwa penalti.
    Mwaka jana Serengeti Girs ilitolewa pia na Copper Princesses katika hatua kama hii ya kufuzu Kombe la Dunia kwa kuchapwa 5-0 Lusaka Februari 3, kabla ya kushinda 1-0 Dar es Salaam hapo hapo Chamazi Februari 11.
    Ikumbukwe Serengeti Girls ni timu pekee ya soka Tanzania iliyowahi kucheza Fainali za Kombe la Dunia – ilikuwa mwaka 2022 nchini India ambako ilifika hadi Robo Fainali na kutolewa na Colombia kwa kuchapwa 3-0.
    Katika Kundi lake ilishinda 2-1 dhidi ya Ufaransa, kabla ya kutoa sare ya 1-1 na Canada kufuatia kufungwa 4-0 na Japan katika mchezo wa kwanza – hivyo kumaliza na pointi nafasi ya pili nyuma ya Japan iliyomaliza na pointi tisa na wote kufuzu Robo Fainali.
    Kwa upande wao, Canada walimaliza na pointi mbili ya tatu na Ufaransa waliomaliza na pointi moja wakashika mkia.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERENGETI GIRLS YATOLEWA KUFUZU KOMBE LA DUNIA KWA VIPIGO ‘DABO’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry