MWANAMUZIKI wa muziki wa kizazi kipya, Raymond Shaban Mwakyusa maarufu Rayvanny ametangazwa kuwa balozi wa kampuni ya michezo ya kubashiri matokeo ya Pigabet.
Mkurugenzi mkuu wa Pigabet, Panayiotis Giannakopoulos amesema wameingia mkataba wa Rayvanny kutokana na kuvutiwa na kazi zake mbalimbali za muziki na kuwa na chapa kubwa katika fani hiyo.
Akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Kula Shavu uliofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam, Giannakopoulos amesema mwanamuziki huyo atakuwa balozi wa kampeni hiyo ambayo inakwenda kutoa fursa kwa wananchi kuibuka na ushindi kila siku.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Pigabet, Panayiotis Giannakopoulos (kushoto) akimkabidhi jezi balozi wao mpya, mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Raymond Shaban Mwakyusa maarufu kwa jina la Rayvanny wakati wa uzinduzi rasmi wa promosheni ya “Kula Shavu” uliofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
“Mkataba wetu na Rayvanny ni wa muda mrefu, ambao umezingatia vigezo, kama kampuni tumaamini tutafikia lengo letu," amesema.
Amessma Pigabet ni kampuni ya Tanzania hivyo inawapa fursa Watanzania kucheza na kushinda.
Akizungumzia namna Wananchi watakavyonufaika na promosheni hiyo, Rayvanny amesema, promosheni ya Kula Shavu inatoa fursa kwa watanzania kupata burudani ya kipekee na kuongeza kipato.
“Pigabet imekuja kivingine mwaka huu na kwa wote watakao jisajili kwa mara ya kwanza kwa kutumia kodi ya CHUI watapata bashiri za bure zenye thamani ya Sh30,000 kila mmoja,” amesema.
Amesema ili kushiriki katika promosheni hii wateja wote wa “kizazi cha wajanja” watacheza kwa dau la kuanzia Sh2,000 na kubashiri mechi mbili au zaidi, na jumla ya odds zisizopungua 2.5 ili kuingia kwenye nafasi ya ushindi kila wiki na katika droo kubwa ya mwisho wa mwezi.
“Tutakuwa na washindi 10 ambao kila mmoja atashinda Sh500,000 kila wiki na droo kubwa mwisho wa mwezi itakayotoa washindi watano ambao kila mmoja atajinyakulia kitita cha Sh2 milioni.
" Tunatarajia kuwa na jumla ya washindi 300 kwa mwezi mmoja,” amesema.
Amizungumzia nafasi ya ubalozi, Rayvanny amesema anajisikia faraja kubwa kufanya kazi na Pigabet kutokana na ukweli kuwa ni kampuni ya kisasa yenye malengo ya kuleta maendeleo hapa nchini.
“Ni faraja kwangu, kwani kama mnavyojua, huwa si saini mikataba na kampuni ambazo hazina tija, hivyo ni fursa kwangu na kwa Watanzania kucheza na kushinda kupitia promosheni hii,” amesema
0 comments:
Post a Comment