TIMU ya Pamba Jiji FC ya Mwanza imefanikiwa kutinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mashujaa FC.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, bao pekee la Pamba Jiji limefungwa na kiungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Alain Mukeya dakika ya 45’+2.
Pamba inakamilisha idadi ya timu nane zilizofuzu Robo Fainali za Kombe la TFF katika mwaka wa pili tu wa udhamini was CRDB — nyingine ni mabingwa watetezi, Yanga, Simba, Singida Black Stars, Kagera Sugar, Mbeya City, JKT Tanzania na Kagera Sugar.
0 comments:
Post a Comment