MABINGWA watetezi, Yanga wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Songea United jioni ya Leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga leo yamefungwa na kiungo Mkenya, Duke Ooga Abuya dakika ya 22 na winga Mkongo, Jonathan Ikangalombo dakika ya 54 wote wakimalizia kazi nzuri za kiungo Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua.
0 comments:
Post a Comment