TIMU ya KMC imeibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya wenyeji, Azam FC katika mchezo wa kirafiki usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mabao ya KMC leo yamefungwa na Deusdedit Cosmas Okoyo dakika ya 19, Shaaban Iddi Chilunda dakika ya 48, Redemtus Mussa dakika ya 56 na Akram Muhina Omar dakika ya 82, wakati ya Azam FC yamefungwa na Zidane Sereri dakika ya 13 na Tepsi Evans dakika ya 89.
0 comments:
Post a Comment