// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ZANZIBAR HEROES YACHAPWA 1-0 NA BURKINA FASO KOMBE LA MAPINDUZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ZANZIBAR HEROES YACHAPWA 1-0 NA BURKINA FASO KOMBE LA MAPINDUZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, January 07, 2025

    ZANZIBAR HEROES YACHAPWA 1-0 NA BURKINA FASO KOMBE LA MAPINDUZI


    WENYEJI, Zanzibar usiku wa Jumatatu wamechapwa bao 1-0 na Burkina Faso katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea Uwanja wa Gombani, Pemba, Zanzibar.
    Bao pekee la The Stallions lililoizamisha Zanzibar Heroes usiku wa jana lilifungwa na Hanabi Hadalou dakika ya 74 na sasa Burkina Faso inaongoza ligi ya michuano hiyo kwa pointi zake nne kuelekea mechi yake ya mwisho na Tanzania Bara.
    Zanzibar Heroes wanabaki nafasi ya pili kwa pointi zao tatu walizovuna kwenye ushindi wa 1-0 dhidi ya ndugu zao, Kilimanjaro Stars kwenye mchezo wa ufunguzi.
    Michuano hiyo inaendelea leo kwa mchezo mwingine mmoja, Tanzania  Bara dhidi ya jirani zao, Kenya.
    Wakati Kilimanjaro Stars ilichapwa 1-0 na Zanzibar Heroes kwenye mechi ya ufunguzi — Harambee Stars waliłazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na The Stallions.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZANZIBAR HEROES YACHAPWA 1-0 NA BURKINA FASO KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top