KLABU ya Yanga imeweka hai matumaini ya kufuzu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al-Hilal Omdurman ya Sudan leo Uwanja wa Cheikha Ould Boidiya Jijini Nouakchott nchini Mauritania.
Bao pekee la Yanga katika mchezo wa leo limefungwa na kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki dakika ya saba baada ya kupokea pasi ya beki Dickson Nickson Job.
Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi saba, ingawa inabaki nafasi ya tatu nyuma ya Al Hilal yenye pointi 10 na MC Alger ya Algeria pointi nane, wakati TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemolrasia ya Kongo (DRC) yenye pointi mbili inashika mkia.
Mechi za mwisho Yanga watakuwa wenyeji wa MC Alger Jumamosi ijayo kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Benjamin Mkapa na mshindi wa mchezo huo afaungana na Al-Hilal Omdurman kwenda Robo Fainali.
Kwa MC Alger hata sare itawasogeza hatua inayofuata ya michuano hiyo.
0 comments:
Post a Comment