TIMU ya Tanzania Bara imekamilisha mechi zake tatu za Kombe la Mapinduzi kwa kupoteza zote baada ya leo pia kuchapwa mabao 2-0 na Burkina Faso Uwanja wa Gombani, Pemba, Zanzibar.
Mabao yaliyoiteketeza Kilimanjaro Stars leo yamefungwa na Abdoulkarim Baguian dakika ya 30 na Clement Pitroipa dakika ya 42 na kwa ushindi huo The Stallions inafikisha pointi saba na kuendelea kuongoza ligi ya michuano hiyo.
Kenya ‘Harambee Stars’ inafuatia nafasi ya pili kwa pointi zake nne, ikifuatiwa na wenyeji, Zanzibar wenye pointi tatu.
Zanzibar Heroes na Harambee Stars watakamilisha Hatua ya awali ya michuano hiyo kwa mchezo baina yao utakaoanza Saa 1:15 usiku hapo hapo Uwanja wa Gombani.
Ikumbukwe mshindi wa kwanza na wa pili ndio watakaokutana katika Fainali Januari 13, hapo hapo Uwanja wa Gombani.
0 comments:
Post a Comment