TIMU ya Simba SC imefanikiwa kutinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika licha ya sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Bravos do Maquis katika mchezo wa Kundi A leo Uwanja wa Novemba 11 Jijini Luanda nchini Angola.
Kiungo Muafrika Kusini, Keoikantse Abednego Mosiatlhaga alianza kuifungia Bravos do Maquis dakika ya mshambuliaji Mcameroon, Christian Leonel Ateba Mbida kuisawazishia Simba dakika ya 69.
Mechi nyingine ya Kundi A Kombe la Shirikisho leo, wenyeji CS Constantine wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia Uwanja wa Mohamed-Hamlaoui Jijini Constantine, Algeria.
Kuelekea mechi za mwisho, CS Constantine yenye pointi 12 na Simba SC pointi 10 zote zimefuzu Robo Fainali, wakati Bravos do Maquis yenye pointi saba inaungana na Sfaxien ambayo haina pointi kuishia Hatua ya 16 Bora.
0 comments:
Post a Comment