NYOTA wa zamani wa soka Afrika Mashariki, Hassan Wasswa wa Uganda, Mrisho Ngassa wa Tanzania na McDonald Mariga wa Kenya wameteuliwa kuwa Wasaidizi wa Droo ya upangaji wa Ratiba ya Fainali za Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) Jumatano.
Droo hiyo ya Fainali hizo zinazoandaliwa kwa pamoja na nchi Kenya, Tanznaia na Uganda zitakazofanyika kuanzia Februari 1 hadi 28 itafanyika Jumatano kuanzia Saa 11:00 jioni ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi, Kenya.
Timu zilizofuzu kushiriki Fainali hizo pamoja na wenyeji, Kenya na Tanzania na Uganda - nyingine ni Morocco, Sudan, Niger, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Zambia, Burkina Faso, Guinea, Nigeria, DRC, Rwanda, Angola, Senegal, Madagascar, Kongo Brazzaville na Mauritania.
0 comments:
Post a Comment