// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC YAICHAPA TANZANIA PRISONS 4-0 MWENGE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC YAICHAPA TANZANIA PRISONS 4-0 MWENGE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, December 22, 2024

    YANGA SC YAICHAPA TANZANIA PRISONS 4-0 MWENGE


    MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam.
    Mabao ya Yanga leo yamefungwa na wazawa, mshambuliaji Clement Francis Mzize dakika ya 13, beki Ibrahim Hamad Abdullah ‘Bacca’ mawili dakika ya 42 na 83 na mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 45.
    Kwa matokeo hayo, Yanga inafikisha pointi 33 katika mchezo wa 13 na kusogea nafasi ya pili, ikiizidi tu wastani wa mabao Azam FC ambayo pia imecheza mechi mbili zaidi.
    Wote wapo nyuma ya Simba SC yenye pointi 34 za mechi 13 pia, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake 11 za mechi 15 sasa nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitateremka daraja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YAICHAPA TANZANIA PRISONS 4-0 MWENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top