UONGOZI wa Shirikisho la Mchezo wa Bao Tanzania (SHIMBATA) umemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kumsaidia gharama za matibabu Rais wa Shirikisho hilo Monday Likwepa.
Ombi hilo limetolewa Leo na mjumbe wa SHIMBATA Sheikh Rashid Kayumbo wakati akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa msaada huo ni gharama za kusaidiwa matibabu ya ndani na nje ya nchini ambapo kwa sasa yupo kitengo cha moyo Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .
" Huyu ndiye mtanzania pekee aliyeshikiria ndoto, maono na kiu ya Hayati mwl Julius Nyerere kuhakikisha kwamba mchezo wa bao unafanikio na kuwa katika orodha ya michezo mikubwa kimataifa Duniani kote," alisema Kayumbo.
Alisema kuwa maono hayo ni pamoja na kuuenzi mchezo wa bao sambamba na kutaka kufanya uwe katika orodha ya utamaduni Bora kimataifa.
Aliongeza kuwa Kwa jitihada zake binafsi amefanikiwa kwenda kuipeperusha ya Tanzania kimataifa iliyofanyika Septemba mwaka huu Kazakstani.
"Mimi naweza kusimama Kam shujaa na mzalendo wa kweli Kwa sababu nilisimama na kila hatua nilitoa ushirikiano na tukafanikiea vyema kuitangaza vyema nchini ," aliongeza .
0 comments:
Post a Comment