TIMU ya Simba SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Lilikuwa ni bao la dakika ya 90 na ushei la mkwaju wa penalti wa Kiungo Muivory Coast, Jean Charles Ahoua aliyemchambua kipa Yacoub Suleiman wa JKT Tanzania baada ya beki Mohamed Bakari kumchezea rafu Shomari Kapombe kwenye boksi.
JKT Tanzania ikamaliza mechi pungufu ya mchezaji mmoja baada ya Refa Kayombo Kefa wa Mbeya kumtoa kwa kadi nyekundu Mohamed Bakari kufuatia kumuonyesha kadi ya pili ya njano alipomchezea rafu Shomari Kapombe.
Kwa ushindi huo, Simba inafikisha pointi 37 katika mchezo wa 14 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu, mbele ya mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 33 za mechi 13, wakati JKT Tanzania inabaki na pointi zake 19 za mechi 15 sasa nafasi ya nane kwenye ligi ya timu 16.
0 comments:
Post a Comment