TIMU ya taifa ya vijana Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imefanikiwa kukata tiketi ya AFCON U17 2025 nchini Morocco baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Sudan Kusini Uwanja wa Hamz, zamani Nakivubo Jijini Kampala katika Nusu Fainali ya kwanza ya michuano ya CECAFA U17.
Mabao ya Serengeti Boys yamefungwa na Abel Joasiah, Ng'habi Zamu, Hussein Mbegu na Juma issa sasa Serengeti Boys itakutana na wenyeji, Uganda walioitoa Somalia kwa kuichapa 2-1 jioni ya leo hapo hapo Uwanja wa Hamz.
Fainali itachezwa Ijumaa kuanzia Saa 6:30 mchana, huku zote Uganda na Tanznaia zikiwa zimejikatia Tiketi ya AFCON U17 2025 nchini Morocco.
0 comments:
Post a Comment