KOCHA wa JKT Tanzania, Ahmad Ally amepewa jukumu la kukiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza kuanza Januari 3, mwakani Uwanja wa Gombani, Pemba.
Tayari Kocha huyo ameteua wachezaji 28 kuunda kikosi cha Kilimanjaro Stars kitakachoingia kambini kujiandaa na michezo ya Kombe la Mapinduzi 2025.
Mbali na Tanzania Bara, timu nyingine zinazotarajiwa kushiriki michuano hiyo ni wenyeji, Zanzibar, Kenya, Uganda, Burundi na Burkina Faso.
Bingwa wa michuano hiyo ambayo hii itakuwa mara ya kwanza kushirikisha timu za taifa baada ya kuwa kushirikisha klabu tangu ilipoanzishwa mwaka 2007 — atazawadiwa Fedha Sh. Milioni 100.
0 comments:
Post a Comment