BAO la dakika ya 90‘+5 la mshambuliaji Maulid Shaaban limeipa Coastal Union ushindi wa 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Katika mchezo huo ulioanza Saa 7:00 mchana wa leo baada ya kuahirishwa jana kutokana na mvua iliyoharibu mandhari ya Uwanja jana – Coastal Union walitangulia kwa bao la beki wa kushoto Mkongo, Hernest Briyock Malonga dakika ya 42 kwa penalti.
Lakini mshambuliaji mzawa, Meshack Abraham Mwamita akaisawazishia Tanzania Prisons dakika ya 56 – lakini ndoto za Maafande kujapa pointi moja leo zikazimwa na Mau mtoto wa mzee wa Shebby.
Kwa ushindi huo, Coastal Union wanafikisha pointi 16 katika mchezo wa 13 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake 10 za mechi 12 sasa nafasi ya 13.

0 comments:
Post a Comment