TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku wa jana Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mabao ya Azam FC yalifungwa na mshambuliaji Nassor Saadun Hamoud dakika ya 11, kiungo Feisal Salum Abdallah kwa penalti dakika ya 45’+3 na Dickson Mhilu aliyejifunga dakika ya 60, wakati bao pekee la Dodoma Jiji alijifunga pia beki Mkongo, Yanick Litombo Bangala dakika ya saba.
Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 30 katika mchezo wa 13 na kurejea kileleni mbele ya Simba yenye pointi 28 na Yanga 27 baada ya wote kucheza mechi 11, wakati Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 16 za mechi 13 pia nafasi ya tisa.
0 comments:
Post a Comment