TIMU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jana ilifanikiwa kutwaa taji Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, AS FAR Rabat Uwanja wa Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan nchini Morocco.
Shujaa wa TP Mazembe, timu kutoka Jiji la Lubumbashi alikuwa ni kiungo fundi mwenye umri wa miaka 28, Marlène Kasaj Yav aliyefunga bao hilo pekee kwa mkwaju wa penalti dakika ya 10 na hilo linakuwa taji la kwanza kwao kihistoria la michuano hiyo likiwafuta machozi ya kutolewa hatua ya makundi 2022.
Kwa ushindi huo, TP Mazembe wamezawadiwa Dola za Kimarekani 600,000, huku washindi wa pili AS FAR wakizawadiwa Dola 400,000.
Ikumbukwe juzi FC Masar ilifanikiwa kumaliza nafasi ya tatu baada ya ushindi wa kwa penalti 4-3 dhidi ya Edo Queens ya Nigeria kufuatia sare ya bila mabao Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan nchini Morocco.
0 comments:
Post a Comment