TANZANIA imetupwa nje ya mbio za kuwania tiketi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) kwa penalti 6-5 na Sudan baada ya sare ya jumla ya 1-1.
Mechi ya kwanza Jumapili iliyopita Sudan walishinda 1-0 Uwanja wa Cheikha Ould Boïdiya Jijini Nouakchott nchini Mauritania.
Na leo mchezo wa marudiano Taifa Stars imeshinda 1-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam bao pekee la mshambuliaji Crispin Ngushi dakika ya 34, kabla ya mchezo kuhamia kwenye mikwaju ya penaltı na Sudan wakasonga mbele.
Sudan sasa atakutana na mshindi wa jumla kati ya Ethiopia na Eritrea mwezi Desemba katika hatua ya mwisho ya mchujo wa tiketi ya CHAN, ingawa Tanzania kama Kenya na Uganda zimekwishafuzu kwa tiketi ya uenyeji.
0 comments:
Post a Comment