VIGOGO, Simba SC wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Pamba Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Bao pekee la Simba leo limefungwa na mshambuliaji Mcameroon, Christian Leonel Ateba Mbida kwa mkwaju wa penalti dakika ya 23 kufuatia yeye mwenyewe kuangushwa kwenye boksi na beki Mkenya wa Pamba Christopher Oruchum ambaye pia ni Nahodha.
Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 28 katika mchezo wa 11 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi nne zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC ambao pia wana mechi moja mkononi.
Kwa upande wao, Pamba Jiji baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao nane mechi 12 sasa nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka daraja.

0 comments:
Post a Comment