WENYEJI, Simba Sports wameanza vyema hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Bravos do Maquis jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini dar es Salaam.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo chipukizi wa umri wa miaka 22, Jean Charles Ahoua kwa mkwaju wa penalti ya kiwango cha juu cha ujuzi dakika ya 27.
Ahoua, mchezaji bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Ivory Coast - alimchambua kipa mkongwe wa miaka 34 wa Angola, Landú Mavanga – kufuatia beki wa Bravos, Samuel Neves Bengue kuokoa kwa mkono mpira wa juu kwenye boksi dhidi ya mshambuliaji Mganda, Steven Dese Mukwala.
Dakika tatu baada ya kuanza kipindi cha pili, kipa Mguinea wa Simba, Moussa Camara aliokoa mkwaju wa penalti wa mshambuliaji Mnigeria wa Bravos do Maquis, Emmanuel Edmond na kuwanusuru wenyeji kuruhusu bao.
Mechi nyingine ya Kundi A iliyoanza Saa 1:00 usiku huu inaendelea Uwanja wa Olimpiki Hammadi-Agrebi mjini Rades, Tunisia muda huu baina ya wenyeji, CS Sfaxien na CS Constantine.
Simba watakuwa na mchezo mmoja wa Ligi Kuu dhidi ya Singida Black Stars ugenini Jumapili, kabla ya kusafiri kwenda Algeria kwa ajili ya mchezo wa pili wa Kundi A Kombe la Shirikisho Desemba 8 Uwanja wa Mohamed-Hamlaoui mjini Constantine.

0 comments:
Post a Comment