KOCHA Hemed Suleiman ‘Morocco’ amemuita mshambuliaji Simon Msuva anayechezea klabu ya Al-Talaba yenye maskani yake Al-Rusafa, Baghdad nchini Iraq kwenye kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania.
Pamoja na Msuva, wachezaji wengine waliorejeshwa Taifa Stars ni makipa, Aishi Salum Manula wa Simba SC na Metacha Boniphace Mnata wa Singida Black Stars.
Taifa Stars itakuwa na michezo miwili ya mwisho ya Kundi H dhidi ya Ethiopia Novemba 16 Uwanja wa Stade des Martyrs, Jijini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na dhidi ya Guinea Novemba 19 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Kwa sasa Taifa Stars inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne nyuma ya Guinea yenye pointi sita na DRC ambao wamekwishafuzu baada kwa pointi zao 12.
Kikosi kamili cha Taifa Stars kinaundwa na makipa:
Aishi Manula (Simba SC), Metacha Mnata (Singida Black Stars) na Zuberi Foba (Azam FC).
Mabeki: Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Paschal Msindo (Azam FC), Shomari Kapombe (Simba SC), Mohamed Hussein (Simba), David Bryson (JKT Tanzania), Ibrahim Hamad (Yanga SC), Dickson Job (Yanga SC), Ibrahim Ame (Mashujaa FC) na Abdulrazak Hamza (Simba SC).
Viungo: Adolf Mtasingwa (Azam FC), Novatus Dismas (Gotzepe, Uturuki), Habib Khalid (Singida Black Stars), Mudathir Yahya (Yanga) na Feisal Salum (Azam FC).
Washambuliaji: Mbwana Samatta (PAOK FC, Ugiriki), Clement Mzize (Yanga), Kibu Dennis (Simba SC), Simon Msuva (Al-Talaba, Iraq), Iddi Suleiman (Azam FC), Ismail Mgunda (Mashujaa FC), Abdulkarim Kiswanya (Azam FC U20), Nassor Saadun (Azam FC) na Cyprian Kachwele (Vancouver Whitecaps, Canada).
0 comments:
Post a Comment