MABINGWA watetezi, Yanga SC wamekutana na kipigo cha pili mfululizo baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Hadi mapumziko Tabora United walikuwa wanaongoza 2-0, mabao yote yakifungwa na nyota mzawa, Offen Francis Chikola mawili dakika za 19 na 45’+4 mara zote akimalizia pasi za kiungo mwenzake mshambuliaji, Yacouba Songe.
Chikola alifunga bao la pili kwa shambulizi la kujibu baada ya kipa Hussein Masalanga kudaka mkwaju wa penalti wa kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki uliotolewa kufuatia kiungo Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua kuangushwa kwenye boksi.
Kipindi cha Tabora walipata bao la tatu lililofungwa na kiungo Mkongo, Nelson Omba Munganga dakika ya 78 akimalizia pasi ya mshambuliaji mzawa, Ibrahim Ahmada ‘Hilika', kabla ya mshambuliaji mwingine mzawa, Clement Francis Mzize kuifungia Yanga bao la kufutia machozi dakika ya 90’+5 akimalizia pasi ya mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo.
Kwa ushindi huo, Tabora United inafikisha pointi 17 katika mchezo wa 11 na kusogea nafasi ya sita, wakati Yanga inabaki na pointi zake 24 nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na watani, Simba baada ya wote kucheza mechi 10.

0 comments:
Post a Comment