// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TAIFA STARS YACHAPWA 1-0 NA DRC KUFUZU AFCON - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TAIFA STARS YACHAPWA 1-0 NA DRC KUFUZU AFCON - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, October 10, 2024

    TAIFA STARS YACHAPWA 1-0 NA DRC KUFUZU AFCON


    TIMU ya taifa ya Tanzania imefungwa bao 1-0 na wenyeji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa Kundi H kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 usiku huu Uwanja wa Martyrs de la Pentecôte, zamani Kamanyola Jijini Kinshasa.
    Mshambuliaji wa Yanga SC, Clement Francis Mzize alijikuta anamfunga kipa wake, Ally Salim Juma Khatoro wa Simba dakika ya 53 katika jitihada za kuokoa.
    Kwa ushindi huo, Chui wa DRC wanafikisha pointi tisa na kuendelea kuongoza Kundi H wakifuatiwa na Taifa Stars yenye pointi nne za baada ya wote kucheza mechi tatu.
    Taifa Stars wanarejea nyumbani kwa ndege yao waliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hasan kwa ajili mchezo wa marudiano Jumanne Uwanja wa Benjamin Jijini Dar es Salaam.
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAIFA STARS YACHAPWA 1-0 NA DRC KUFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top