// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TABORA UNITED YAZINDUKIA KWA PAMBA, YAICHAPA 1-0 MWINYI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TABORA UNITED YAZINDUKIA KWA PAMBA, YAICHAPA 1-0 MWINYI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, October 23, 2024

    TABORA UNITED YAZINDUKIA KWA PAMBA, YAICHAPA 1-0 MWINYI


    TIMU ya Tabora United imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Pamba Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
    Ni mkwaju wa penalti wa kiungo Mnigeria, Morice Ugochukwu Chukwu dakika ya 77 uliotolewa baada ya beki Samson Madeleke kumchezea rafu mshambuliaji Mburkinabe, Yacouba Sogne.
    Kwa ushindi huo, Tabora United wanafikisha pointi 11 na kusogea nafasi ya saba, wakati Pamba Jiji inabaki na pointi zake tano nafasi ya 15 baada ya wote kucheza mechi tisa.
    Ni mchezo wa pili kwa kocha Freddy Felix Minziro tangu akabidhiwe mikoba Pamba Jiji kufuatia kufukuzwa kwa Mserbia, Goran Kopunovic – lakini bado mambo si shwari kwani mechi ya kwanza alilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Kagera Sugar, nyumani Mwanza. 

    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TABORA UNITED YAZINDUKIA KWA PAMBA, YAICHAPA 1-0 MWINYI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top