// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SHIME AITA 23 TWIGA STARS KUCHEZA NA MOROCCO NA SENEGAL - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SHIME AITA 23 TWIGA STARS KUCHEZA NA MOROCCO NA SENEGAL - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, October 06, 2024

    SHIME AITA 23 TWIGA STARS KUCHEZA NA MOROCCO NA SENEGAL


    KOCHA Bakari Nyundo Shime ameita wachezaji 23 kuunda kikosi ha timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki dhidi ya Morocco ma Senegal baadaye mwezi huu.
    Katika kikosi hi hicho ameita wachezaji 11 wanaocheza nje na wengine 12 wanatoka klabu za Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, ingawa hakuna hata mmoja wa Yanga Princess.
    Wanaocheza nje ni pamoja Nahodha, Opa Clement wa Henan FC ya China, Aisha Masaka wa Brighton & Hove Albion ya England, Malaika Meena wa Wake Forest ya Marekani, Diana Lucas wa Ame S.F.K. ya Uturuki, Enekia Kasonga wa Mazatlanfemenil na Juletha Simgano wa Juarez zote za Mexico.
    Wengine ni Noela Luhala wa ASA Tel Aviv ya Israel, Maimuna Kaimu wa ZED FC, Hasnat Ubamba wa FC Masar za Misri na Clara Luvanga ya Al Nassr ya Saudi Arabia.
    Wanaocheza nyumbani ni Najat Abbas, Lidya Maximilian, Christer Bahera, Stumai Abdallah, Winifrida Gerald, Yasinta Mitoga wa JKT Queens, Asha Mrisho wa Amani Queens, Janet Shija, Vaileth Nicholaus wa Simba Queens, Melikia Williams, Esther Maseke na Victoria Masele wote wa Bunda Queens. 
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SHIME AITA 23 TWIGA STARS KUCHEZA NA MOROCCO NA SENEGAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top