// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NGORONGORO HEROES YAICHAPA SUDAN 1-0 CECAFA U20 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NGORONGORO HEROES YAICHAPA SUDAN 1-0 CECAFA U20 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, October 10, 2024

    NGORONGORO HEROES YAICHAPA SUDAN 1-0 CECAFA U20


    TANZANIA imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sudan katika mchezo wa Kundi A za Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA U20 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
    Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo wa Yanga, Shekhan Abdallah Khamis dakika ya 76 na kwa ushindi huo, Ngorongoro Heroes inayofundishwa na Kocha mkongwe, Charles Boniface Mkwasa inafikisha pointi sita baada ya kucheza mechi tatu.
    Ngorongoro sasa ndio inaongoza Kundi A kwa wastani wa mabao dhidi ya Sudan ambayo imecheza mbili, wakati Kenya yenye pointi nne za mechi mbili inashika nafasi ya tatu ikifuatiwa na Rwanda yenye pointi moja kufuatia kucheza mechi mbili na Djibouti iliyofungwa mechi zake zote mbili za awali inashika mkia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGORONGORO HEROES YAICHAPA SUDAN 1-0 CECAFA U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top