// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC YAUWASHA MOTO, YAITANDIKA KEN GOLD 4-1 CHAMAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC YAUWASHA MOTO, YAITANDIKA KEN GOLD 4-1 CHAMAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, October 25, 2024

    AZAM FC YAUWASHA MOTO, YAITANDIKA KEN GOLD 4-1 CHAMAZI


    WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa mabao 4-1 Ken Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
    Mabao ya Azam FC Leo yamefungwa na kiungo Feisal Salum dakika ya 20 kwa penalti, mshambuliaji Mcolombia, Jhonier Blanco dakika ya 37, winga Mgambia, Gibril Sillah dakika ya 50 na beki Msenegal, Cheikh Sidibe dakika ya 72, wakati bao pekee la Ken Gold limefungwa na mshambuliaji Ibrahim Joshua Mwakasaba kwa penalti dakika ya 87.
    Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 18 na kusogea nafasi ya nne, wakati Ken Gold iliyopanda Ligi Kuu msimu huu inabaki na pointi zake nne na kuendelea kushika nafasi ya mwisho, ya 16 katika msimamo baada ya wote kucheza mechi tisa.
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAUWASHA MOTO, YAITANDIKA KEN GOLD 4-1 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top