// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC YATINGA MAKUNDI SHIRIKISHO, WALIBYA ‘WAFA’ 3-1 KWA MKAPA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC YATINGA MAKUNDI SHIRIKISHO, WALIBYA ‘WAFA’ 3-1 KWA MKAPA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, September 22, 2024

    SIMBA SC YATINGA MAKUNDI SHIRIKISHO, WALIBYA ‘WAFA’ 3-1 KWA MKAPA


    WENYEJI, Simba SC wamefanikiwa kutinga Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya katika mchezo wa marudiano Hatua ya 32 Bora jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    Haukuwa ushindi mwepesi kwa Simba, kwani walilazimika kutoka nyuma baada ya kutanguliwa na Ahli kwa bao la mshambuliaji wa Kimataifa wa Angola, Agostinho Cristovao Paciencia ‘Mabululu’ dakika ya 17.
    Mshambuliaji mzawa, Kibu Dennis Prosper alianza kuifungia Simba bao zuri la kusawazisha kwa tik-tak dakika ya 36, kabla ya mshambuliaji Mcameroon, Christian Leonel Ateba Mbida kufunga bao la pili dakika ya 45’+1 na winga mzawa Edwin Charles Balua akafunga la tatu dakika ya 90.
    Kwa matokeo hayo, Simba inakwenda hatua ya 16 Bora ambayo huchezwa kwa makundi kufuatia sare ya bila mabao kwenye mchezo wa kwanza Jumamosi iliyopita Jijini Tripoli. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YATINGA MAKUNDI SHIRIKISHO, WALIBYA ‘WAFA’ 3-1 KWA MKAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top