// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PAMBA JIJI WATOA SARE YA 2-2 NA MASHUJAA CCM KIRUMBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PAMBA JIJI WATOA SARE YA 2-2 NA MASHUJAA CCM KIRUMBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, September 21, 2024

    PAMBA JIJI WATOA SARE YA 2-2 NA MASHUJAA CCM KIRUMBA


    WENYEJI Pamba Jiji FC wamelazimishwa sare ya kufungana mabo 2-2 na Mashujaa FC ya Kigoma katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
    Pamba ilikuwa inaongoza 2-0 hadi dakika 10 za mwisho kwa mabao ya Saleh Abdallah dakika ya 32 na John Nakibinge dakikaya 40, kabla ya Mashujaa kusawazisha kupitia kwa Richard Ulomi aliyefunga mabao yote dakika ya 76 na 84.
    Kwa matokeo hayo, Pamba Jiji inafikisha pointi tatu katika mchezo wa tano, tatu za awali ikitoa sare za 0-0 na Tanzania Prisons, Dodoma Jiji na Azam FC na kufungwa moja na Singida Black Stars 2-1.
    Kwa upande wao Mashujaa inafikisha pointi nane katika mchezo wa nne, tatu za awali ikishinda mbili, 1-0 zote dhidi ya Dodoma Jiji na Coastal Union na sare ya bila mabao na Tanzania Prisons.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PAMBA JIJI WATOA SARE YA 2-2 NA MASHUJAA CCM KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top