// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); FOUNTAIN GATE YAICHAPA KAGERA 3-1 NA KUPANDA KILELENI LIGI KUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE FOUNTAIN GATE YAICHAPA KAGERA 3-1 NA KUPANDA KILELENI LIGI KUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, September 27, 2024

    FOUNTAIN GATE YAICHAPA KAGERA 3-1 NA KUPANDA KILELENI LIGI KUU


    WENYEJI, Fountain Gate wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati, Manyara.
    Mabao ya Fountain Gate yamefungwa na Suleiman Mwalimu dakika ya sita, Salum Kihimbwa dakika ya 11 na Mkongo Ellie Mokono dakika ya 90’+4, wakati la Kagera Sugar limefungwa na Mzambia, Obrey Chirwa dakika ya 50.
    Kwa ushindi huo, Fountain Gate inafikisha pointi 13 katika mchezo wa sita na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ikiizidi Singida Black Stars pointi moja, ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi.
    Mambo yanazidi kuwa magumu kwa Kagera Sugar, kwani sasa inafikisha mechi sita za kucheza, lakini inabaki na pointi zake nne tu. 
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FOUNTAIN GATE YAICHAPA KAGERA 3-1 NA KUPANDA KILELENI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top