• HABARI MPYA

    Tuesday, July 02, 2024

    URENO NA UFARANSA KATIKA ‘BONGE LA ROBO FAINALI’ EURO 2024


    TIMU za Ufaransa na Ureno usiku wa jana zimefanikiwa kwenda Hatua ya Robo Fainali Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2024 baada ya kuzitoa Ubelgiji na Slovenia nchini Ujerumani.
    Ilianza Ufaransa kuitupa nje Ubelgiji kwa bao la kujifunga la beki wa Anderlecht, Jan Bert Vertonghen dakika ya 85 Uwanja wa Dusseldorf Arena Jijini Düsseldorf.
    Na baadaye Ureno wakalazimika kusubiri mikwaju ya penalti kuitoa Slovenia kwa 3-0 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120, tena Nahodha wake Cristiano Ronaldo akikosa penalti dakika ya 105 ambayo iliokolewa na kipa Jan Oblak.
    Shujaa wa Ureno alikuwa kipa Diogo Costa aliyeokoa penalti zote tatu za Slovenia zilizopigwa na Josip Iličić, Jure Balkovec na Benjamin Verbič.
    Waliofunga penalti tatu za Ureno ni Cristiano Ronaldo, Bruno Fernandes na Bernardo Silva na sasa watakutana na Ufaransa katika Robo Fainali Ijumaa.
    Hatua ya 16 Bora Euro 2024 inakamilishwa leo kwa michezo miwili zaidi, Romania na Uholanzi Saa 1:00 usiku na Austria dhidi ya Uturuki Saa 4:09 usiku.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: URENO NA UFARANSA KATIKA ‘BONGE LA ROBO FAINALI’ EURO 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top