// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); RED ARROWS MABINGWA KOMBE LA KAGAME, AL HİLAL WA TATU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE RED ARROWS MABINGWA KOMBE LA KAGAME, AL HİLAL WA TATU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, July 21, 2024

    RED ARROWS MABINGWA KOMBE LA KAGAME, AL HİLAL WA TATU


    TIMU ya Red Arrows ya Zambia imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame kwa ushindi wa penalti 10-9  dhidi ya APR ya Rwanda kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 Leo Uwanja wa Manispaa ya Kinondoni (KMC) Jijini Dar es Salaam.
    Mshambuliaji Ricky Banda alianza kuifungia Red Arrows dakika ya 62, kabla ya mshambuliaji wa Kimataifa wa Mauritania kuisawazishia APR dakika ya 90.
    Na kwenye mikwaju ya penalti ikawa bahati ya waalikwa kutoka ukanda wa Kusini kwa Afrika (COSAFA) kutwaa taji la michuano hiyo iliyodhaminiwa na Mamlaka ya Bandari Dar es Salaam.
    Mapema mchana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu Al Hilal Omdurman ilishinda kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya dhidi ya Hay Al Wad Nyala, zote za Sudan hapo hapo Uwanja wa KMC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RED ARROWS MABINGWA KOMBE LA KAGAME, AL HİLAL WA TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top