// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PRINCE DUBE AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO YANGA IKIICHAPA GALAXY 1-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PRINCE DUBE AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO YANGA IKIICHAPA GALAXY 1-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, July 24, 2024

    PRINCE DUBE AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO YANGA IKIICHAPA GALAXY 1-0


    BAO la mshambuliaji mpya, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 55 limeipa Yanga ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, TS Galaxy katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Kanyamazane mjini Mpumalanga nchini Afrika Kusini.
    TS Galaxy ikipoteza nafasi nzuri ya kusawazisha bao hilo baada ya kiungo nyota wa timu hiyo Siphesihle Maduna kupiga nje mkwaju wa penalti, ambao hata hivyo kipa wa Kimataifa wa Mali, Djigui Diarra aliufuata.
    Huo unakuwa mchezo wa pili wa kujpima kwenye kambi yao ya Afrika Kusini baada ya kuchapwa 2-1 na Augsburg ya Ujerumani Jumamosi iliyopita Uwanja wa Mbombela, huko huko Mpumalanga.
    Yanga SC watakamilisha mechi zake za kujipima kwenye kambi yao ya wiki mbili Afrika Kusini kujiandaa na msimu kwa kucheza na Kaizer Chiefs Jumapili, Julai 28 Uwanja wa Toyota mjini Bloemfontein, kabla ya kurejea nchini kwa ajili ya Kilele cha Wiki ya Mwananchi Agosti 4 na baadaye mechi ya Ngao dhidi ya Simba Agosti 8 Uwanja wa Mkapa.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PRINCE DUBE AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO YANGA IKIICHAPA GALAXY 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top