// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HIZI HAPA JEZI ZA MSIMU MPYA SIMBA ZIMEZINDULIWA MIKUMI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HIZI HAPA JEZI ZA MSIMU MPYA SIMBA ZIMEZINDULIWA MIKUMI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, July 24, 2024

    HIZI HAPA JEZI ZA MSIMU MPYA SIMBA ZIMEZINDULIWA MIKUMI


    HATIMAYE vigogo wa soka, Simba Sports Club leo wamezindua jezi za msimu mpya wa 2024 – 2025, shughuli ambayo imefanyika Hifadhi ya Mikumi mkoani Morogoro na kuhudhuriwa na mamia ya mashabiki wa timu hiyo waliosafiri kwa Treni ya mwendo kasi, SGR kutoka Dar es Salaam. 
    Jezi hizo zimetolewa na Kampuni ya Sandaland The Only One, ambao wapo katika mwaka wao wa pili wa udhamini wa jezi kwa Wekundu hao wa Msimbazi, kufuatia mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Sh. Bilioni 2 uliosainiwa Juni 16 mwaka jana Jijini Dar es Salaam.
    Kwa sasa kikosi cha Simba kimeweka kambi mjini Ismailia nchini Misri kujiandaa na msimu mpya ambao wataufungua kwa mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya watani, Yanga Agosti 8 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HIZI HAPA JEZI ZA MSIMU MPYA SIMBA ZIMEZINDULIWA MIKUMI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top