// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); JAMIE VARDY MCHEZAJI BORA TENA WA MWEZI ENGLAND, RANIERI AWA KOCHA BORA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE JAMIE VARDY MCHEZAJI BORA TENA WA MWEZI ENGLAND, RANIERI AWA KOCHA BORA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, December 11, 2015

    JAMIE VARDY MCHEZAJI BORA TENA WA MWEZI ENGLAND, RANIERI AWA KOCHA BORA

    MSHAMBULIAJI Jamie Vardy ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Novemba Ligi Kuu ya England.
    Ametwaa tena tuzo hiyo, baada ya kufunga mabao matatu katika mechi za mwezi Novemba, ikiwemo ya kuvunja rekdi katika sare ya 1-1 na Manchester United. 
    Bao lake la kwanza dakika ya 24 dhidi ya Mashetani Wekundu lilimfanya avunje rekodi ya Ruud van Nistelrooy kwa kufunga kwenye mechi 11 mfululizo za Ligi Kuu.

    Vardy (kulia) na kocha wake, Claudio Ranieri wakiwa na tuzo zao baada ya kukabidhiwa leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    Wote, Vardy na kocha wake, Claudio Ranieri, ambaye ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Ligi Kuu Novemba, wamepewa heshina iliyotokana na kazi yao nzuri Leicester katika Ligi Kuu.
    Leicester imeshinda mechi mbili kati ya tatu November na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu baada ya mechi 15, mechi yao iliyopita wakiifunga Swansea 3-0 Uwanja wa Liberty, siku ambayo Vardy hakufunga baada ya kufunga mara 11 mfululizo. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JAMIE VARDY MCHEZAJI BORA TENA WA MWEZI ENGLAND, RANIERI AWA KOCHA BORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top