// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC IMEKAMILIKA KUELEEKEA MCHEZO NA MGAMBO, HAJIB WA MABAO NA BEKI LA NGUVU HASSAN ISIHAKA WAMEPIGA MATIZI LEO TANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC IMEKAMILIKA KUELEEKEA MCHEZO NA MGAMBO, HAJIB WA MABAO NA BEKI LA NGUVU HASSAN ISIHAKA WAMEPIGA MATIZI LEO TANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, September 14, 2015

    SIMBA SC IMEKAMILIKA KUELEEKEA MCHEZO NA MGAMBO, HAJIB WA MABAO NA BEKI LA NGUVU HASSAN ISIHAKA WAMEPIGA MATIZI LEO TANGA

    Na Princess Asia, TANGA
    WACHEZAJI wawili nyota wa Simba SC, beki Hassan Isihaka (pichani juu) na mshambuliaji Ibrahim Hajib wamefanya mazoezi na timu yao leo mjini hapa kuelekea mchezo wa Jumatano dhidi ya JKT Mgambo.
    Wote Hajib na Isihaka walikosa mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji African Sports Jumamosi Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kutokana na kuwa majeruhi.
    Lakini kuelekea mchezo wa keshokutwa dhidi ya JKT Mgambo utakaopigwa Mkwakwani pia, Nahodha Msaidizi Isihaka na mshambuliaji tegemeo la mabao, Hajib wamerudi.
    Daktari wa Simba SC, Yassin Gembe ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo kwamba wachezaji wote hao wamefanya mazoezi vizuri kabisa leo kuelekea mchezo wa Jumatano.
    “Sasa ni suala la mwalimu mwenyewe kuamua kuwapanga au la, lakini suala la maumivu halipo tena,”amesema Dk Gembe.
    Ibrahim Hajib (kushoto) naye yuko fiti kuwavaa JKT Mgambo Jumatano

    Mchezaji pekee aliyebaki majeruhi kati ya waliosafiri na Simba SC Tanga ni beki Samih Hajji Nuhu, wakati viungo Jonas Mkude na Abdi Banda hawakusafiri kabisa na timu. 
    Kocha Muingereza wa Simba SC, Dyla Kerr ameanza vizuri Ligi Kuu baada ya kuiongoza timu yake kushinda 1-0 dhidi ya Sports Jumamosi Uwanja wa Mkwakwani na keshokutwa atajaribu kutimiza pointi sita katika mechi mbili za mwanzo ugenini. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC IMEKAMILIKA KUELEEKEA MCHEZO NA MGAMBO, HAJIB WA MABAO NA BEKI LA NGUVU HASSAN ISIHAKA WAMEPIGA MATIZI LEO TANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top