// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC, YANGA AZAM ZAPEWA MUDA ZAIDI KUSAJILI…SASA DIRISHA KUFUNGWA AGOSTI 20 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC, YANGA AZAM ZAPEWA MUDA ZAIDI KUSAJILI…SASA DIRISHA KUFUNGWA AGOSTI 20 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, August 06, 2015

    SIMBA SC, YANGA AZAM ZAPEWA MUDA ZAIDI KUSAJILI…SASA DIRISHA KUFUNGWA AGOSTI 20

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesogeza mbele tarehe ya mwisho ya usajili wa wachezaji kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili hadi Agosti 20, mwaka huu.
    Awali, dirisha la usajili lilikua lifungwe leo Agosti 6, na usajili mdogo wa ndani ungefungwa Septemba 5, 2015 lakini sasa usajili wote kwa jumla utafungwa Agosti 20, 2015.
    Tarehe 21- 28 Agosti, 2015 ni kipindi cha pingamizi, tarehe 29-30 Agosti 2015, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itapitia na kupitisha usajili.


    Kiungo Mzimbabwe Justice Majabvi yupo Tanzania kwa ajili ya kusajiliwa Simba SC

    Dirisha la uhamisho wa wachezaji wa Kiamataifa (FIFA –TMS) litafungwa tarehe 06 Septemba, 2015 na Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 12, 2015.
    TFF imezitaka klabu kukamilisha usajili huo katika muda huo uliowekwa, ili kupunguza usumbufu wa kufanya usajili dakika za mwisho,na dirisha litakapofungwa Agosti 20, litafunguliwa tena wakati wa dirisha dogo mwezi Novemba 15 mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC, YANGA AZAM ZAPEWA MUDA ZAIDI KUSAJILI…SASA DIRISHA KUFUNGWA AGOSTI 20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top