// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIVUMBI KAGAME 2015 CHAANZA LEO DAR, MAGUFULI KUSHUHUDIA ‘TIMBWILI’ LA YANGA NA GOR MAHIA UWANJA WA TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIVUMBI KAGAME 2015 CHAANZA LEO DAR, MAGUFULI KUSHUHUDIA ‘TIMBWILI’ LA YANGA NA GOR MAHIA UWANJA WA TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, July 18, 2015

    KIVUMBI KAGAME 2015 CHAANZA LEO DAR, MAGUFULI KUSHUHUDIA ‘TIMBWILI’ LA YANGA NA GOR MAHIA UWANJA WA TAIFA

    Yanga SC wanafungua dimba na Gor Mahia ya Kenya leo Kombe la Kagame

    RATIBA KOMBE LA KAGAME 2015

    Julai 18, 2015
    KMKM vs Telecom           
    APR  Vs  Shandy               
    Yanga Vs Gor Mahia       
    Julai 19, 2015
    LLB AFC Vs Hegaan FC  
    Adama City Vs Malaika
    Azam Vs KCCA                 
    Julai 20, 2015
    Telecom Vs Khartoum 
    Gor Mahia Vs KMKM 
    Julai 21, 2015
    Shandy Vs LLB AFC      
    Hegaan Vs  APR   
    Malaika Vs Azam        
    Julai 22, 2015
    Khartoum Vs KMKM
    KCCA Vs Adama City
    Telecom Vs Yanga    
    Julai 23, 2015
    Hegaan Vs Shandy
    APR Vs LLB AFC     
    Julai 24, 2015
    Khartoum Vs Gor Mahia
    KMKM Vs Yanga
    Julai 25, 2015
    KCCA Vs Malakia
    Adama City Vs Azam    
    Julai 26, 2015
    Gor Mahia Vs Telecom    
    Yanga Vs Khartoum     
    Julai 27, 2015 MAPUMZIKO
    Julai 28, 2015 ROBO FAINALI
    B1 Vs A3
    A1 Vs Mshindi wa tatu Bora
    Julai 29, 2015
    B2 Vs C2
    C1 Vs A2
    Julai 29, 2015 MAPUMZIKO
    Julai 31, 2015 NUSU FAINALI
    Mshindi 25 Vs Mshindi 26
    Mshindi 23 Vs Mshindi 24
    Agosti 1, 2015 MAPUMZIKO
    Agosti 2, 2015 
    MSHINDI WA TATU NA FAINALI
    Aliyefungwa 27 Vs Aliyefungwa 28
    Mshindi 27 Vs Mshindi 28
    Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIPYENGA cha michuano ya 40 ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kinapulizwa leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Kutakuwa na mechi tatu katika siku ya kwanza leo kwenye viwanja viwili tofauti, kwanza KMKM ya Zanzibar na Telecom ya Djibouti kuanzia Saa 8:00 mchana na baadaye wenyeji Yanga SC dhidi ya Gor Mahia ya Kenya Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, muda ambao pia APR ya Rwanda itamenyana na Al Shandy ya Sudan Uwanja wa Karume.
    Waziri wa Ujenzi, Dk John Pombe Joseph Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa michuano hiyo na mgombea huyo wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (CCM) atawasili muda mfupi kabla ya mechi rasmi ya ufunguzi wa Kagame ya 40 kuanza, kati ya Yanga na Gor. 
    Michuano hiyo ina makundi matatu, A likijumuisha timu za Yanga SC, KMKM, Telecom na Gor Mahia wakati wenyeji wengine, Azam FC wapo Kundi C pamoja na Malakia ya Sudan Kusini, Adama City ya Ethiopia na KCCA ya Uganda na Kundi B kuna APR ya Rwanda, Al-Shandy ya Sudan, LLB AFC ya Burundi na Heegan FC ya Somalia.
    Azam FC itafungua dimba na KCCA Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Saa 10: 00 jioni mchezo utakaotanguliwa na mechi nyingine kati ya Adama City na Malakia utakaonza Saa 8:00 mchana, wakati jioni Saa 10:00 Uwanja wa Karume, LLB AFC itamenyana na Hegaan FC.
    Mabingwa wa michuano hiyo, El Merreikh ya Sudan hawakuja kutetea taji, kwa sababu wapo kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Sudan, El Hilal pia nao hawajaja kwa kuwa wapo kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. 
    Simba SC ndiyo timu iliyotwaa mara nyingi zaidi Kombe la Kagame

    ORODHA YA MABINGWA NA WASHINDI WA PILI KOMBE LA KAGAME
    MwakaNchiBingwaMatokeoMshindi wa piliNchiMwenyeji





    1974 TanzaniaSimbaAbaluhya Kenya Tanzania
    1975 TanzaniaYoung Africans2–0Simba Tanzania Zanzibar
    1976 KenyaLuo Union2–1Young Africans Tanzania Uganda
    1977 KenyaLuo Union2–1Horsed Somalia Tanzania
    1978 UgandaKampala City Council0–0*[C]Simba Tanzania Uganda
    1979 KenyaAbaluhya1–0Kampala City Council Uganda Somalia
    1980 KenyaGor Mahia3–2Abaluhya Kenya Malawi
    1981 KenyaGor Mahia1–0Simba Tanzania Kenya
    1982 KenyaA.F.C. Leopards1–0Rio Tinto Zimbabwe Kenya
    1983 KenyaA.F.C. Leopards2–1ADMARC Tigers Malawi Zanzibar
    1984 KenyaA.F.C. Leopards2–1Gor Mahia Kenya Kenya
    1985 KenyaGor Mahia2–0A.F.C. Leopards Kenya Sudan
    1986 SudanAl-Merrikh2–2*[D]Young Africans Tanzania Tanzania
    1987 UgandaVilla1–0Al-Merrikh Sudan Uganda
    1988 KenyaKenya Breweries2–0Al-Merrikh Sudan Sudan
    1989 KenyaKenya Breweries3–0Coastal Union Tanzania Kenya
    1990
    Mashindano hayakufanyika[E]
    1991 TanzaniaSimba3–0Villa Uganda Tanzania
    1992 TanzaniaSimba1–1*[F]Young Africans Tanzania Zanzibar
    1993 TanzaniaYoung Africans2–1Villa Uganda Uganda
    1994 SudanAl-Merrikh2–1Express Uganda Sudan
    1995 TanzaniaSimba1–1*[G]Express Uganda Tanzania
    1996 TanzaniaSimba1–0Armée Patriotique Rwandaise Rwanda Tanzania
    1997 KenyaA.F.C. Leopards1–0Kenya Breweries Kenya Kenya
    1998 RwandaRayon Sports2–1Mlandege Zanzibar Zanzibar
    1999 TanzaniaYoung Africans1–1*[H]Villa Uganda Uganda
    2000 KenyaTusker3–1Armée Patriotique Rwandaise Rwanda Rwanda
    2001 KenyaTusker0–0*[I]Oserian Kenya Kenya
    2002 TanzaniaSimba1–0Prince Louis Burundi Zanzibar
    2003 UgandaVilla1–0Simba Tanzania Uganda
    2004 RwandaArmée Patriotique Rwandaise3–1Ulinzi Stars Kenya Rwanda
    2005 UgandaVilla3–0Armée Patriotique Rwandaise Rwanda Tanzania
    2006 UgandaPolice2–1Moro United Tanzania Tanzania
    2007 RwandaArmée Patriotique Rwandaise2–1Uganda Revenue Authority Uganda Rwanda
    2008 KenyaTusker2–1Uganda Revenue Authority Uganda Tanzania
    2009 SudanATRACO1–0Al-Merrikh Sudan Sudan
    2010
    Mashindano hayakufanyikadagger[J]
    2011 TanzaniaYoung Africans1–0Simba Tanzania Tanzania
    2012 TanzaniaYoung Africans2–0Azam Tanzania Tanzania
    2013 BurundiVital'O2–0A.P.R. Rwanda Sudan
    2014 SudanAl-Merrikh1–0A.P.R. Rwanda Rwanda
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIVUMBI KAGAME 2015 CHAANZA LEO DAR, MAGUFULI KUSHUHUDIA ‘TIMBWILI’ LA YANGA NA GOR MAHIA UWANJA WA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top