WAKATI Cristiano Ronaldo anawasili kwa mara ya kwanza kutoka Lisbon katika Jiji la Manchester, wachache walikuwa wanafahamu kuhusu kijana huyo mwenye kipaji akiwa nywele zake zenye njano kwa mbali.
Lakini kutokana na kuonyesha uwezo mkubwa, sasa amekuwa mmoja wa wachezaji wakubwa duniani- nyota huyo anayevaa jezi namba 7 Real, amekuwa kioo kwa wengi.
Acha tuwe wakweli, kama unaweza kukimbia kama yeye, kupiga mashiti na vichwa, huwezi kujali mengine
Mapokezi mazuri: Cristiano Ronaldo (kulia) alitambulishwa kama mchezaji wa Man United, Agosti 13, mwaka 2003 na kocha Sir Alex Ferguson na mchezaji mwenzake mpya Kleberson
Ronaldo haraka aliibuka silaha kubwa ya Manchester United na kipenzi cha mashabiki
Siku Kuu: Ronaldo akishangilia bao la kwanza katika fainali ya Kombe la FA mwaka 2004 FA, ambayo United ilishinda 3-0 dhidi ya Millwall kwenye Uwanja wa Millenium
Chini: Ronaldo (juu) ilibidi ajifunze kuhimili rafu, hapa akiangushwa chini na Wayne Rooney wa Everton, ambaye baadaye alijiunga naye United.
Winga wa Ureno, Ronaldo kulia akiugulia maumivu katika Euro 2004baada ya kufungwa 1-0 na Ugiriki katika fainali
Kocha wa Ureno, Luiz Felipe Scolari (kulia) akimfuta machozi Ronaldo baada ya kuumizwa na kipigo cha Ugiriki.
MAFANIKIO YA RONALDO MAN UNITED
TUZO:
Ligi Kuu (06-07, 07-08, 08-09)
Kombe la FA (03-04)
Kombe la Ligi (05-06, 08-09)
Ligi ya Mabingwa (07-08)
Ngao ya Jamii (07)
Klabu Bingwa ya Dunia (08)
P140 W105 D23 L12 Win% 75
Mabao 72 (asilimia 0.51 kwa mechi)
Ligi Kuu 57 Ligi ya Mabingwa 8 Kombe la FA 4 Kombe la Ligi 3
Baada ya kujiunga na Manchester United mwaka 2003 kwa dau la pauni Milioni 12, Ronaldo alipata mafanikio makubwa akiwa na Mashetani hao Wekundu, ikiwemo kutwaa Kombe la FA katika msimu wake wa kwanza akifunga bao la kwanza katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Millwall kwenye fainali.
Ronaldo pia alikuwa ndiye mchezaji aliyefunga bao la 1000 la United katika Ligi Kuu, Oktoba mwaka 2005.
Pia alishinda tuzo ya FIFPro ya Mchezaji Maalum Kinda wa mwaka katika msimu huo.
Hakusubiri muda mrefu kushinda taji lingine, baada ya kuwa miongoni mwa nyota waliotwaa Kombe la Ligi msimu wa 2005-06, United ikiifunga Wigan 4-0 katika fainali.
Lakini licha ya kuonyesha uwezo mkubwa, bado alikuwa anakabiliwa na mtihani wa kumudu mchezo wa nguvu na rafu katika soka ya England.
Uchezaji wa Ronaldo ulikuwa wa mbinu zaidi na ujanja mwingi, ambao haukuwa na madhara sana.
Msimu uliofuata alibadilika mno na kuanza kuendana na kashikashi za England, na haikuwa ajabu alipofanikiwa kufunga mabao 20 msimu huo na kushinda mfululizo tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi.
Msimu wa 2007-08 ulikuwa mzuri kwa Ronaldo Manchester United.
Ronaldo akifunga bao la ushindi dhidi ya Wigan katika fainali ya Kombe la Ligi mwaka 2006, United ikishinda 4-0
Ronaldo akionyeshwa kadi ya njano kwa kuvua jezi wakati akishangilia bao
Ronaldo akifurahia maisha na Kocha Sir Alex Ferguson enzi hizo Man United
Alishinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia baada ya kufunga mabao 31 Ligi Kuu, kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufunga moja ya mabao yake ya kukumbukwa dhidi ya Portsmouth. Ulikuwa ni msimu ambao dunia ilimtambua yeye ni nani.
Baada ya msimu mmoja zaidi Manchester, akifunga mabao 26 katika klabu hiyo, aliuzwa kwa dau la rekodi ya dunia, Pauni Milioni 80 kwenda Real Madrid.
Tangu ajiunge na vigogo hao wa Ulaya, ameweza kufunga mabao 136 katika mechi 126, ingawa amekuwa akikabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa Muargentina wa Barcelona, Lionel Messi, dunia inajiuliza nani zaidi… Messi au Ronaldo?
Ronaldo amekuwa nyota ndani na nje ya uwanja
Ronaldo akiota jua katika ufukwe wa nyumba ya Malibu, ambako dakika 30 tu tangu atokeze kutoka ndani tayari alizungukwa na vimwana kibao
Msimu wa 2007-08 ulikuwa mzuri sana kwa Ronaldo katika maisha yake Old Trafford, kwa mshambuliaji huyo kufunga mabao 42 katika mechi 49
Ronaldo (kushoto) akiwa na tuzo yake ya Mchezaji Bora kinda wa PFA na Mchezaji Bora wa Mwaka na kocha wake, Alex Feguson na tuzo maalum ya Special Merit mwaka 2007
Cristiano Ronaldo (katikati) akitibiwa baada ya kuumizwa kichwani hadi kutoka damu katika mechi dhidi ya Roma. Ilibidi wachezaji wa timu pinzani wamchezee sana rafu ili kumpunguza makali
Ronaldo akipokea kiatu cha Dhahabu baada ya kujfunga mabao 31 katika Ligi kwenye mechi 34 msimu wa 2007-2008 - alifunga karibu katika kila mechi aliyocheza
Ferguson na Ronaldo wakiwa na tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka wa PFAaliyoshinda Mreno huyo akiwa na United mwaka 2008
Cristiano Ronaldo akitembea kusalimia mashabiki wakati wa kutambulishwa kwake Real Madrid baada ya kuuzwa kwa pauni Milioni 80
Ronaldo akivua jezi yake kushangilia kuifungia Real Madrid - anaonekana tofauti na mchezaji aliyetua Old Trafford akiwa kinda